Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Hai linaloongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Irene Lema amekanusha taarifa ya kupokonywa ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo kama ilivyotangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Katibu huyo, amesema kuwa Freeman wa Mbowe hajawahi kutumia ofisi yeyote iliyopo ndani ya Halmashauri ya Hai kutokana na kuwa na wageni wengi huku chumba cha halmashuri kikishindwa kuhudumia idadi ya wageni hao.

Aidha, amesema kuwa Mbunge huyo hana ofisi ndani ya Halmashauri ya Hai, na aliamua kuweka nje ya halmashauri kwa sababu ilikuwa ni ndogo na akaamua kuweka nje ili kuwapokea wageni wengi wanaotoka ndani na nje ya jimbo.

“Ofisi yetu iko wazi muda wote na ninavyokwambia muda huu nimetoka kukutana na watu watatu ambao wanashida na Mbunge, kwa hiyo ofisi yetu tunashirikiana vizuri sana na wafanyakazi wote wa halmashauri ya Hai akiwemo Mkurugenzi tena bila kujali vyama vyao,” amesema.

Hata hivyo, mapema wiki hii, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya alitangaza kumpokonya Freeman Mbowe ofisi yake, akidai kuwa kiongozi huyo hajaonekana katika ofisi yake kwa muda mrefu.

 

Video: JPM amzungumzia mrithi mikoba yake, Zitto ageuka kituko bungeni
RC Kagera awawekea mikakati Madereva Bodaboda