Ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za ukadiriaji kodi kwa wakati, Serikali imeagiza ofisi zote za ardhi nchini kutoa huduma siku zote za juma hadi mwisho wa mwezi aprili.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ametoa agizo hilo leo Februari 7, 2023 Jijini Dodoma na kuwataka wananchi kuendelea kutumia njia za ki-elekroniki ambazo zimeanza kutolewa na Benki washirika za CRDB na NMB katika kukadiria na kulipa kodi.

Amesema, Rais Dkt. Samia ameongeza muda wa msamaha wa riba ya malimbikizo hivyo wananchi wanapaswa kuchangamkia msamaa huo na kwamba Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imejipanga kuwahudumia, ili kuwawezesha kupata nafuu ya msamaha wa riba ya pango la ardhi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula.

Aidha, Mabula pia amesisitiza kuwachukulia hatua za kisheria kwa kukusanya kodi na malimbikizo ya wananchi, mashirika na kampuni ambazo hazita tumia msamaha huo kwa kuubatilisha milki, kuwafikisha mahakamani, kukamata mali na kunadi, ili kufidia kodi stahiki.

“Natoa rai kwa taasisi na mashirika ya umma na wananchi wote kutumia muda uliotolewa hadi April 30 na Mhe. Rais kunufaika na msamaha wa riba uliotolewa na Serikali kulipa deni la msingi (principal amount) ili wasamehewe riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi,” amesema.

Kamati TPLB yatengua maamuzi
Uteuzi: Wanane wateuliwa ujumbe wa Bodi TAFORI