Viongozi wakuu wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) wamesema wanaitambua Jerusalem kama mji wa Palestina na kwamba hawatakubali kuona hilo likibadilika, wakiitaka Marekani kufuta msimamo wake.

Viongozi hao wameitaka Marekani kufuta uamuzi wake mara moja wa kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, huku wakitishia kuchukuwa hatua kali dhidi ya Marekani na Israel endapo wataendelea na mipango yao ya kuufanya mji huo mtukufu kwa dini zote tatu – Ukritso, Uislamu na Uyahudi – kuwa makao makuu ya Israel.

Aidha, Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesema kuwa uamuzi wa Marekani kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel ni uhalifu, huku akisema kuwa mji huo sio sehemu ya Marekani hivyo Donald Trump hana mamlaka ya kutoa maamuzi yeyote.

“Haitakubalika tena kwa Marekani kuwa na jukumu lolote kwenye mchakato wa kisiasa kwa sababu imeegemea upande mmoja wa Israel. Huo ndio msimamo wetu na tunataraji nanyi mutatuunga mkono.”amesema Abbas

Hata hivyo, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, mwenyeji Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema kuwa anabeba jukumu la kuitangaza rasmi Jerusalem kuwa mji mkuu wa Palestina huku akitaka uungwaji mkono wa viongozi wengine wa Kiislamu duniani.

LIVE: Kuagwa kwa Mashujaa waliopoteza maisha DRC
Vyama vya Siasa vyazidi kuwavuruga wananchi