Baada ya kukamilisha mpango wa kujiunga na Simba SC usiku wa kuamkia jana Alhamis, Kiungo kutoka nchini Nigeria Nelson Okwa amefunguka na kuweka wazi matarajio yake ndani ya klabu hiyo ya Msimbazi.

Okwa amesajiliwa Simba SC akitokea nchini kwao Nigeria alikokua akiitumikia klabu ya Rivers United iliyocheza dhidi ya Young Africans msimu uliopita, na kuwafunga Wananchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 amesema, amejiunga na Simba SC ili kufanikisha malengo ya klabu hiyo, na pia kwa upande wake kama mchezji ambaye anaamini bado ana nafasi kubwa ya kuendelea kucheza soka kwa mafaikio makubwa Afrika ama nje ya Bara hilo.

Amesema amechagua kuitumikia Simba SC baada ya kuifuatilia kwa muda mrefu na kujiridhisha ni mahala sahihi ambapo patamuwezesha kufikia ndoto zake kama mchezaji.

“Ni changamoto nyingine mpya katika maisha yangu ila naamini nitakuwa na msimu mzuri hapa Simba SC kutokana na uwezo wangu pamoja na ushirikiano nitakaoupata kutoka kwa wachezaji wenzangu, kwa hakika Wanasimba watafurahi.”

“Kabla sijasajiliwa hapa, niliijua Simba SC kutokana na kufanya vizuri kwenye Michuano ya Kimataifa, najua kila hatua waliokuwa wanaipiga kwenye Michuano hiyo, nakumbuka walikuja nyumbani Nigeria wakacheza na Plateau United na kushinda bao 1-0.”

“Hata nilipokuja hapa msimu uliopita nikiwa na Rivers United kwa ajili ya mchezo wetu na Young Africans, bado niliifuatilia Simba SC na pia nilisikia mengi sana kuihusu klabu hii, hivyo ilipofikia hatua ya viongozi kuhitaji huduma yangu sikusita, kwa sababu ninaifahamu klabu hii.” amesema Okwa.

UNESCO yataka uchunguzi mauaji Mwandishi wa Habari
Serikali kujikita na utatuzi shida za Wananchi