Msanii wa muziki wa hip hop nchini Nigeria, Olamide Adebeji, ameweka wazi kuwa kwa miaka 17 sasa amekuwa akiishi bila ya mwanamke na kuamua kuufanya muziki ni sehemu ya maisha yake.

Msanii huyo amedai kuwa, maamuzi hayo yalifuatiwa na hali ya maisha yaliyokuwa yakimkabili msanii huyo, kwani aliishi maisha ya kimaskini  na kuamua kuachana na mambo ya wanawake kwa miaka 17 iliyopita na kujikita katika muziki.

”Ni wazi kwamba sina mwanamke kwa miaka 17 sasa, niliamini kuwa ningefuata wanawake kwa sasa nisingeweza kufanikiwa, lakini kwa sasa nina mafanikio makubwa kutokana na muziki, hivyo naweza kusema kwa kipindi chote hicho mke wangu ni muziki”

”Nilikuwa na lengo la kuja kuishi maisha mazuri, nashukuru nimeweza kutimiza malengo yangu, lakini kama ningefuata wanawake nisingeweza,” amesema Olamide”.

Olamide ameenda kinyume na msemo usemao palipo maendelendeleo ya mwanaume basi kuna mwanamke nyuma ya hayo maendeleo, wanawake wengi wamekuwaa na msukumo mkubwa katika mafanikio ya wanaume lakini kwa Olamide imekuwa tofauti anaamini mwanamke ni chanzo cha umaskini hivyo katika kipindi cha kuyatafuta maendeleo yake hakutaka kujihusisha na wanawake.

 

 

Salum Chama: Mwamuzi Wa Simba Vs Yanga Atajulikana Kesho
Video: "Serikali hii ni sikivu" - Majaliwa