Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka ameiagiza halmashauri ya mji wa Njombe kuwachukulia hatua watumishi waliosababisha hasara halmashauri hiyo.

Ole Sendeka ametoa maagizo hayo mkoani Njombe katika kikao cha baraza maalumu la madiwani wa halmashauri ya mji wa Njombe ili kujadili hoja za mkaguzi wa hesabu za serikali.

“Natarajia ripoti ambayo mkurugenzi utaleta kwa katibu tawala na ofisini kwangu, ili niunganishe na halmashauri nyingine sita pamoja na ofisi yangu kwa pamoja nipeleke ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa lakini ripoti hiyo iwe imeainisha majina ya waliosababisha hoja, vyeo vyao na hatua za nidhamu zilizochukuliwa”amesema Ole Sendeka

Aidha, halmashauri ya mji wa Njombe imevifikisha mahakamani vikundi 47 vya wajasiriamali ambavyo vimeshindwa kurejesha fedha za mikopo ya asilimia kumi zitokanazo na mapato ya ndani ikiwa na lengo la kuhimiza urejeshwaji ili wahitaji wengine waweze kukopeshwa.

Zaidi ya mil. 98 zimeshindwa kurejeshwa tangu mwaka 2015 hadi sasa jambo ambalo limeibua hoja kwa mkaguzi wa hesababu za serikali CAG ambaye ameshauri halmashauri kuhakikisha zinatoa mikopo hiyo kwa wajasiriamali na kuzifatilia kwa marejesho ili ziweze kutumika kukopesha wahitaji wengine

Kwa upande wake mweka hazina wa halmashauri hiyo, Dorcas Mkello amesema kuwa halmashauri imekuwa na changamoto kubwa katika kufuatilia wadaiwa wa mikopo ya asilimia kumi na kudai kwamba kitendo hicho kimekwamisha mipango ya halmashauri ya kuwawezesha mitaji wajasiriamali

Hata hivyo licha ya halmashauri ya mji wa Njombe kuwa na changamoto nyingi katika utekelezaji wa miradi yake lakini ni miongoni mwa halmshauri tano kati ya sita ambazo zimepata hati safi isipokuwa Makete.

Jenerali Kasike aanza ziara ya kikazi mkoani Kagera
Video: Magufuli amtwisha 'zigo' Kigwangalla, Lissu apata mateso mapya