Ubalozi unapenda kuwajulisha kuwa Serikali ya Oman imeondoa katazo la kuingia Oman kwa abiria kutoka Tanzania na nchi zingine zilizokuwa kwenye kundi hili. 

Aidha kuanzia Septemba 1, 2021 abiria wanaopandia ndege kutoka TAnzanina kuelekea Oman wataruhusiwa kuingia Oman kwa kutimiza baadhi ya masharti ikiwemo kuwa na cheti cha Uviko 19 kinachothibitisha kuwa abiria amekamilisha dozi mbili za chanjo au dozi moja kwa zile ambazo dozi ni moja lakini pia iwe imefanyika sio chini ya siku 14 kabla ya tarehe ya kuingia Oman.

Sharti lingine ni pamoja cheti cha chanjo kuwa na alama ya QR (QR Code), lakini pia chanjo iliytumika lazima iwe miongoni mwa chanjo zilizoidhinishwa nchini humo ikiwemo chanjo ya Johnson and Johnson, AstraZeneca – Oxford.

Koffi Olomide awasili kutumbuiza wiki ya mwananchi
Burna Boy azidi kupasua anga