Msanii wa bongo fleva nchini, Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz kufuatia hali yake ya kiafya kutoridhisha jopo la mashehe mkoani Tabora lilikusanyika nyumbani kwa baba mzazi wa Ommy na kumfanyia dua ya nguvu msanii huyo ili aweze kurejea afya yake.

Siku za hivi karibuni Ommy Dimpoz akiwa nchini Afrika Kusini alifanyiwa upasuaji mkubwa wa koo la chakula na kuwekewa mfumo huo bandia kufuatia tatizo lililokuwa linamsumbua kitambo kidogo la koo lake la chakula kushindwa kupitisha vimiminika na chakula.

Kwa zaidi ya wiki mbili sasa, Dimpoz yupo chini ya uangalizi wa daktari nchini Afrika Kusini baada ya kwenda kufanyiwa vipimo vya maendeleo ya upasuaji wake wa awali wa koo aliofanyiwa miezi mitatu iliyopita.

Ilibainika kuwa, Dimpoz ana tatizo la nyama kuziba kwenye mfumo wa chakula hivyo baada ya kufanyiwa upasuaji, aliwekewa mpira maalum wa kutolea uchafu ambao hadi mwishoni mwa wiki iliyopita, ilishindikana kuutoa kwa sababu bado kidonda kilionekana kuvuja usaha.

Baba wa Dimpoz amekiri kufanya dua hiyo maalum ili mwanaye aweze kupona haraka. Pamoja na kumuombea apone haraka, pia aliomba kama kuna mtu yeyote alishiriki kumpa sumu Mungu amlipe maana yeye ndiye hakimu wa haki.

“Namuombea sana mwanangu na wale waliompa sumu mwaka hautaisha bila Mungu kufanya kitu kwao. “Naumizwa sana na hali ya mwanangu, natamani ugonjwa unaomsumbua uwarudie haohao waliompa sumu ili waone uchungu wake na wao.

“Ukiangalia mwanangu hana hata mtoto wala mke, bado mdogo, kwa nini wamfanyie hivyo? Aliwakosea nini mpaka wampe adhabu kubwa namna hiyo jamani? “Naamini Mungu atawaweka hadharani siku moja na wataumbuka tu,” alisema baba Dimpoz.

Daktari anayemtibu Dimpoz, alisema tatizo la mfumo huo wa chakula lililompata mwanamuziki huyo lilitokana na kuwekewa sumu kwenye kinywaji. Alisema tatizo hilo limeshawatokea wagonjwa wengi aliokutana nao wakiwa kwenye hali mbaya zaidi, lakini kwa mwanamuziki huyo haikuwa kwenye hatua ya kutisha hivyo kuwa na matumaini makubwa ya kumtibu.

Pius Msekwa apongeza juhudi za Rais Magufuli
Pep Guardiola apiga marufuku matumizi ya simu