Ommy Dimpoz ameweka wazi maombi anayopokea kila siku kutoka kwa warembo wakimtaka afunge nao pingu za maisha.

Mwanafamilia huyo wa RockStar 4000 amefunguka kwenye The Playlist ya Times Fm, baada ya kuulizwa kuhusu mpango wake wa kuoa kwani amekuwa mstari wa mbele kuonesha ushirikiano wanapofunga ndoa wasanii wenzake.

Mwimnbaji huyo wa ‘Yanje’ amesema kuwa hawezi kuiga wanachofanya wengine kwani wao walipanga na kufikia uamuzi huo, hivyo anasubiri wakati wake. Lakini aliweka wazi kuwa wakati akiendelea kusubiri amekuwa akipokea maombi kwenye mitandao ya kijamii kupitia ‘inbox’.

“Usikurupuke kwa sababu wengine wamefanya,” alisema Dimpoz. “Unajua hilo swali hata DM yangu sasa hivi iko ‘lit’, mwingine ‘ooh naomba nioe mimi…’ mwingine ‘naomba nikuzalie mtoto basi utanioa baadaye’. Kwahiyo niko bize kupitia zile application (maombi) naangalia niende na yupi,” alifunguka.

Ommy Dimpoz anaendelea kuitangaza ngoma yake mpya ya ‘Yanje’ aliyomshirikisha Sayi Shay, ngoma ambayo imepata mapokezi mazuri.

‘Yanje’ pia imemuibua Ali Kiba ambaye ameahidi kutoa wimbo wake mpya punde wimbo huo wa Ommy Dimpoz utakapotazamwa zaidi ya mara milioni 3 kwenye mtandao wa YouTube.

Waandaaji tuzo za Oscar wawatumbua vigogo kwa ubakaji
Ndege ya kivita ya Urusi yaanguka Syria

Comments

comments