Ongezeko la ulawiti na ubakwaji kwa watoto limeongozeka na kufikia kiasi cha kutishia amani ya maisha yao ya kila siku,Mpaka kufikia hivi sasa Manispaa ya ilala imeunda timu ya ulinzi na usalama wa mtoto inayoratibiwa na Ofisi ya ustawi wa jamii chini ya kitengo cha familia na mtoto kuelekea siku ya mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa tar 16/juni.ambapo kwa mwaka huu kaulia mbiu ni ‘’Ubakaji na Ulawiti wa Watoto vinepukika Chukua Hatua kumlinda mtoto”

Taarifa hiyo imetolewa na Tabu F.Shaibu Afisa uhusiano wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala baada ya wilaya hiyo kuwa na ongezeko kubwa la ubakwaji na ulawiti na ukatili wa watoto ambapo kuanzia februari mwaka huu2016 walibakwa watoto18 na mwezi march ni watoto 26 likiwa ni ongezeko la watoto 8 ndani ya mwezi mmoja

Hata hivyo kuanzia mwaka 2013 Manispaa ya ilala kupitia kituo cha One stop Centre na ofisi za Ustawi wa jamii-hadi march mwaka huu2016 jumla ya watoto 1213 walipatikana na kupewa huduma baada ya kufanyiwa vitendo tofauti vya ukatili.

Aidha watoto 72 wamepatiwa huduma kutoka Madawati ya kijinsia yaliyopo katika kila kituo cha polis,na kati ya hao kessi 23 zipo Mahakamani na kesi 12 teyari zimeshatolewa hukumu za vifungo kwa wahusika,kesi 35 zipo katika hatua tofauti tofauti Ikiwemo hatua za upelelezi wa jeshi la polis kupitia madawati ya jinsia na watoto.

Vilevile timu ya ulinzi na usalama kwa mtoto imeendelea kufanya ufuatiliaji wa kitaaluma Mashuleni kwa watoto Wenye mahitaji maalumu ikiwa ni pamoja na usambazaji wa taarifa kwa waratibu wa elimu wote kutotoza ada na michango mbali mbali kwa watoto hao wenye mahitaji maalumu na wanaoishi mazingira hatarishi.

Pamoja na huduma hizo zinazotolewa kwa watoto hao,mafanikio mengine ni pamoja na kuundwa kwa kamati za kuhudumia watoto walio katika mazingira hatarishi kutoka mitaa 56 ya kata 13,jumla ya watoto25,550(wakike wakiwa13,407 na wakiume ni 12,957) Walio tambuliwa kutoka katika mazingira hatarishi ni pamoja na wanaotoka katika kata za pugu,pugu station,majohe,kiwalani,kipawa,kivule,mchikichini,tabata,kimanga,segerea,bonyokwa,kisukuru na liwiti,jumla ya makao sita ya watoto kati ya 10,yametembelewa na kupatiwa ushauri jinsi ya kuboresha huduma kwa watoto.

Manispaa ya ilala imetoa wito kwa jamiii kutoa taarifa pindi kunapotokea matukio ya aina yoyote ya ukatili wa kijinsia kwa watoto na kuepuka na kuepuka kwa mashauri ya watoto kumalizika kifamilia ili hatua za kisheria zichukuliwe na kumaliza ukatili wa kijinsia kwa watoto katika jamii.

Mwandishi wa hits za Baraka Da Prince adai 'hazimbariki'
Simu feki kupigwa nyundo Leo, Mafundi Simu wanusa Kifungo Jela Miaka 10