Muonekano wa beki wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Joash Abong’o Onyango, umezua mijadala na taharuki  kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusambaa kwa picha yake akiwa katika mwonekano unaodaiwa kuwa haulingani na miaka aliyonayo.

Wadau mbalimbali wa Soka katika mitandao ya kijamii wameonekana kushangazwa na umri wake huku umbo na muonekano wakidai haviendani.

“Huyo jamaa ana miaka 62 na sio 26 hahahaha,” ni maneno ya mmoja wa wadau wa soka anayeitwa MacLean Geofrey ambaye alitoa maoni yake kwenye runinga ya mtandandoni ya dar24 baada ya kutazama video ya habari inayo muhusu Onyango.

Taarifa zinasema mchezaji huyo alizaliwa mwaka 1992, hivi sasa ana umri wa miaka 27, lakini baadhi ya wadau katika mitandao hiyo wamedai kuwa muonekano wake na umri unaotajwa haviendani kwani ni mzee tofauti na miaka yake ilivyo.

Ikumbukwe kuwa Mchezaji huyo sio wa kwanza kuweka mwonekano huo wa kupaka ndevu rangi nyeupe wapo  baadhi ya wachezaji wa Afrika waliomtangulia  katika kuweka staili hiyo ambao ni El Hadji Diouf wa Senegal na Rigobert Song wa Cameroon ambao pia walionekana hivyo kwenye michuano kama hiyo itakayo chezeka nchini Misri.

Harambee Stars wanatarajiwa kuondoka  leo kutoka nchini Ufaransa walipoweka kambi na kuelekea Misri ambapo mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji wa kutumainiwa  na kocha Sebastien Migne kutokana na Brian Mandela kupata majeraha.

Kenya wapo Group C na Algeria, Senegal na Tanzania huku Harambee Stars watachuana na Algeria, Juni 23 wakati siku hiyo, Taifa Stars itacheza na Senegal.

Fahamu ugonjwa hatari wa Ebola
Serikali yaokoa mabilioni uendeshaji mashauri ya madai