Tayari zoezi la kukamata viroba limeanza ambapo maafisa mbali mbali wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Maafisa wa Jeshi la Polisi wapo katika maeneo ya wilaya za Dar es salaam, Temeke, Ilala, Kinondoni na Ubungo ili kuhakikisha kuwa amri iliyotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa inatekelezwa.

Maafisa hao wamefika katika eneo la Mabibo, Dar es salaam katika godauni lililokuwa likitajwa kuhifadhi pombe za viroba na kukuta shehena kubwa ya pombe hizo zikiwa katika makontena.

Mkaguzi wa Vyakula kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), John Mwingira ambaye alikuwa eneo la tukio hilo alisema kuwa kinachofuatia baada ya kukuta shehena hilo ni kuweka ulinzi mkali katika eneo hilo kuhakikisha kwamba pombe hizo hazitoki hadi hapo taratibu nyingine zitakapofuata kama ambavyo maelekezo yalivyotolewa na Serikali.

Kwa upande wake, mmiliki wa godauni hilo lililokutwa na shehena ya pombe hizo amesema kuwa hadi sasa wanasubiri utaratibu wa Serikali kwani wameandika barua wakiomba kuwaongezea muda kwani hadi marufuku hiyo inatolewa tayari wauzaji hao walikuwa na didhaa hizo hivyo wanaiomba Serikali japo iongeze muda wa kufungia pombe hizo.

Michy Batshuayi Kuondoka Stamford Bridge
Max Allegri Aandamwa Safari Ya Emirates Stadium