Saa chache kabla ya kufanyika kwa hafla ya utoaji wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2015, baadhi ya mitandao imeanza kubainisha juu ya kuvuja kwa orodha ya kikosi cha dunia ambacho kitatangazwa katika hafla hilo ambayo itafanyika mjini Zurich nchini Uswiz.

Taarifa za kuvuja kwa matokeo ya hafla ya hii leo zimekua zikichua nafasi kubwa katika mitandao ya habari za michezo duniani kote, na tayari imeshajitokeza kutajwa kwa jina la atakayekuwa mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia kwa mwaka 2015.

Lionel Messi, juma lililopita alitajwa katika mitandao, ambapo inadaiwa taarifa hizo zilivujishwa na baadhi ya maafisa ndani ya FIFA, lakini saa chache baadae shirikisho hilo lilikanusha na kudai jina la mshindi lipo salama.

Muda mcheche uliopita majina ya watakaounda kikosi bora cha mwaka 2015, yameripotiwa kuonekana hadharani na inadaiwa asilimia kubwa kikosi hicho kitaundwa na wachezaji kutoka kwa mabingwa wa soka barani Ulaya na nchini Hispania, FC Barcelona.

Mwandishi wa habari kutoka nchini Hispania, Alfredo Martinez ndiye aliyejitoa muhanga kwa kuanika taarifa hizo katika mtandao wa kijamii wa Twitter, tena akiorodhesha majina ya wachezaji ambao usiku huu yatatajwa katika kikosi bora cha mwaka 2015.

Walio orodheshwa ni mlinda mlango kutoka nchini Italia pamoja na klabu ya Juventus Gianluigi Buffon, Daniel Alves da Silva (Brazil, FC Barcelona), Georgio Chiellini (Italia, Juventus), Sergio Ramos (Hispania, Real Madrid), Marcelo Vieira da Silva Júnior (Brazil, Real Madrid), Andres Iniesta (Hispania, FC Barcelona), James Rodriguez (Colombia, Real Madrid), Paul Pogba (Ufaransa, Juventus), Cristiano Ronaldo (Ureno, Real Madrid), Lionel Messi (Argentina, FC Barcelona) pamoja na Neymar da Silva Santos Júnior (Brazil, FC Barcelona)

Leaked: The FIFA World XI to be announced at the Ballon dOr gala

Harry Kane Aikana Real Madrid
2 Face Idibia abadili jina, Angalia hapa jina lake jipya