Kamati ya Tuzo za VPL, imekamilisha orodha ya awali ya wachezaji 30 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msimu wa mwaka 2017/18, ambayo sherehe zake zitafanyika Juni 23 mwaka huu.

Kila mwezi Kamati ya Tuzo, imekuwa ikitangaza jina la mchezaji aliyefanya vizuri kwa mwezi husika kutokana na vigezo mbalimbali na pia ripoti kutoka kwa makocha waliopo katika viwanja ambavyo ligi hiyo inachezwa.

Wachezaji walioshinda tuzo za mwezi ligi ya msimu huu na miezi yao katika mabano nimshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba). Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John Bocco(Januari), kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari), mshambuliaji wa  Lipuli, Adam Salamba (Machi) na mshambuliaji wa Majimaji, Marcel Kaheza (Aprili).

Wachezaji hao kila mmoja amepewa zawadi ya tuzo, king’amuzi cha Azam na fedha taslimu sh. Mil. Moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.

Hivyo wakati huu tukielekea mwisho wa ligi, leo tunatangaza wachezaji 30 ambao watawania tuzo hiyo, ambao watachujwa na kubaki 10, kisha watabaki watatu ambao ndiyo wataingia fainali ya kuwania tuzo siku ya mwisho.

Wachezaji hao 30 ni

  1.             Habibu Kyombo (Mbao)

 

  1.            Khamis Mcha (RuvuShooting)

 

  1.             Yahya Zayd-Azam

 

  1.             Razack Abalora-Azam

 

  1.             Bruce  Kangwa-Azam

 

  1.             Aggrey Morris -Azam

 

  1.            HimidMao –Azam

 

  1.            Awesu Awesu –Mwadui

 

  1.              Adam Salamba-Lipuli

 

  1.          Mohammed Rashid-Prisons

 

  1.          Shafiq Batambuze-Singida

 

  1.         Mudathir Yahya-Singida United

 

  1.          Marcel Kaheza- Majimaji

 

  1.           Ditram Nchimbi-Njombe Mji

 

  1.         Eliud Ambokile- Mbeya City

 

  1.          Shaaban Nditi-Mtibwa

 

  1.         Tafadzwa Kutinyu-Singida

 

  1.         Ibrahim Ajibu- Yanga

 

  1.         Gadiel Michael-Yanga

 

  1.         Papy Tshishimbi-Yanga

 

  1.          Kelvin Yondani-Yanga

 

  1.         Obrey Chirwa-Yanga

 

  1.        Aishi Manula-Simba

 

  1.        Emmanuel Okwi-Simba

 

  1.        John Bocco-Simba

 

  1.        Jonas Mkude-Simba

 

  1.         Erasto Nyoni-Simba

 

  1.         Shiza Kichuya-Simba

 

  1.         Asante Kwasi –Simba

 

  1.        Hassan Dilunga-Mtibwa

Rais wa Ghana amsweka ndani Mwenyekiti wa Shirikisho la Kandanda
TFF, Vodacom watangaza tarehe ya kutoa tuzo