Mchambuzi wa Soka La Bongo kupitia Kituo cha EFM Radio Oscar Oscar, ameonesha masikitoko yake kufuatia sakata la mvutano wa udhamini wa kampuni ya GSM ambayo inatambulika kama Mdhamini Mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kampuni ya GSM ilisaini Mkataba wa zaidi ya Shilingi Bilioni 2 na Shirikisho la TFF mwezi Novemba kama Mdhamini Mwenza, huku Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara ni Benki ya Taifa ya Biashara ‘NBC’.

Sakata la kuvutana juu ya uhalali wa udhamini wa kampuni ya GSM limepamba moto, baada ya Uongozi wa Simba SC kutangaza hadharani msimamo wao kutokubali kuvaa nembo ya Mdhamini Mwenza kupitia jezi zao za mashindano, hadi utakapotolewa ufafanuzi wa kina kuhusu mkataba uliopo.

Oscar ameyasema hayo mapema leo Jumatano (Desemba 08) akiwa kwenye kipindi cha Sports HQ kilichorushwa na EFM Radio.

Oscar amesema: “Binafsi nimesikitishwa kuona Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi ‘TPLB’, Almas Kasongo kuanza kujibu hoja za Simba maana wao kama Bodi hawakusaini, mkataba ule ni kati ya TFF na GSM group.

“Bodi ya Ligi ni kama kamati ya harusi tu wanatoaje ufafanuzi wa mkataba ambao wao hawakusaini bodi ya Ligi ni kama Simba tu hawafahamu chochote.”

“Bodi ya Ligi inapaswa kuwa huru sio kuwa chini ya mamlaka ya TFF.”

Ndege inayoruhusu mambo ya faragha kufanyika angani
Hassan Dilunga: Ni mchezo wa kawaida, sio DABI