Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius ambaye anatumikia kifungo cha miaka 6 jela, akiwa ameshatekeleza kifungo hicho kwa takribani mwezi mmoja, ameripotiwa kukimbizwa hospitalini baada ya kupata majeraha akiwa Jela.

Kwa mujibu wa AFP, Pistorius aliwaeleza maafisa wa Jeshi la Polisi kuwa alipata majeraha mguuni baada ya kuanguka kutoka kitandani kwake. Imeelezwa kuwa mwanariadha huyo bingwa wa Olympic alikimbizwa katika hospitali moja ya binafsi na baadae kurudishwa jela baada ya kupata matibabu.

Msemaji wa kitengo kimoja cha huduma za jela, Singabakho Nxumalo aliiambia AFP kuwa wanafanya upelelezi kuhusu tukio hilo.

Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka 6 baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mpenzi wake bila kukusudia.

BAVICHA: Tunampenda Magufuli, IGP aandae Polisi kutulinda
Lissu asimulia machungu aliyoyaonja Rumande