Mshambuliaji kutoka nchini Nigeria Victor James Osimhen amesema anaamini SSC Napoli itatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu huu 2022/23.

SSC Napoli imetinga Hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo, baada ya kuichapa Eintracht Frankfurt kwa mabao 3-0, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Diego Armando Maradona mjini Naples, Italia.

Katika mchezo huo Osimhen alifunga mabao mawili huku bao moja likiwekwa kimiani na Piotr Zielinski kwa mkwaju wa penati.

Amesema ana imani timu yake itatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu huu, kutokana na ubora wa wachezaji waliopo kikosini.

Amesisitiza mchezo huo ulikuwa mgumu na wenye upinzani mkali, lakini walipambana kupata ushindi huo ambapo Napoli imefuzu hatua ya Robo Fainali kwa jumla ya mabao 5-0.

“Ninafikiri kila kitu kinawezekana, ndoto zangu ni kuhakikisha ninaendelea kupambana kuisidia timu kupata ushindi katika kila mechi.”

“Ninaamini tunaweza kupata ubingwa wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, kwani tumejipanga vyema ili kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojiwekea.”

“Nitajisikia faraja kwa kuweka rekodi ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwani ni ndoto ya kila mchezaji msimu huu, ninawapongeza wachezaji wote kwa kujituma,” amesema

Msuva, Samatta kuungana na wenzao Misri
Taifa Stars kuondoka Dar kwa mafungu