Beki wa kati kutoka nchini Argentina Nicolas Otamendi, huenda akatangazwa rasmi kuwa mchezaji halali wa klabu ya Man City baada ya kuonekana mjini Manchester, ambapo inaelezwa atafanyiwa vipimo vya afya mjini hapo.

Man city walikubali ada ya usajili wa mchezaji huyo iliyotangazwa na uongozi wa klabu ya Valencia juma lililopita na hatua hiyo iliwapa fursa na kumuandaa kwa safari ya mjini Manchester kufanyiwa vipimo vya afya.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 27, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia Man City, na atakua mchezaji watano kusajiliwa klabuni hapo baada ya Raheem Sterling, Fabian Delph, Enes Unal na Patrick Roberts.

Usajili wa wachezaji hao watano umeigharimu Man City kiasi cha paund million 95, ikiwa ni sehemu ya kiwango kilichotengwa rasmi kwa ajili ya kurejesha heshima ya ubingwa wa England, ambao msimu uliopita alielekea magharibi mwa jijini London kwa wanachelsea.

City wanatarajia kuendeleza wimbi la usajili, mara baada ya kukamilisha taratibu wa Otamendi na anayefuatia ni kiungo kutoka nchini Ublegiji na klabu ya VFL Wolfsburg ya Ujerumani, Kevin De Bruyne ambaye thamani yake ni paund million 50.

Man city tayari wameshaonyesha mwanzo mzuri wa kusaka mafanikio msimu huu, baada ya kuifunga West Brom katika mchezo wa ufunguzi mabao matatu kwa sifuri kisha wakaichabanga Chelsea mabao matatu kwa sifuri na mwishoni mwa juma hili watapambana na Everton.

Otamendi Akamilisha Ndoto Za Kucheza England
Yametimia, Song Kubaki England Jumla