Uvumi wa mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Ufaransa Ousmane Dembele wa kuhamia  Arsenal akitokea FC Barcelona katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi, umeendelea kuchochewa na vyombo vya habari, baada ya mchezaji huyo kupiga picha ya pamoja na wachezaji wa The Gunners baada ya kula nao chakula cha jana jioni.

Dembele yupo jijini London na alikutana na wachezaji Alexandre Lacazette, Matteo Guendouzi, Henrikh Mkhitaryan katika hafla ya chakula cha jioni iliyokua imeandaliwa nyumbani kwa mshambuliaji Emerick Aubameyang.

Baba wa Aubameyang, ameweka picha ya pamoja baina ya wachezjai hao wa Arsenal na mchezaji huyo wa FC Barcelena, katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, na kuzua zogo na shangwe miongoni mwa mashabiki wa soka dunia hususan wale wa The Gunners.

Katika picha hiyo mazazi huyo wa Aubameyang aliandika: ‘Ni fuaraha kuwa na familia ambayo ilijumuika na wachezaji wetu’.

Dembele ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa kombe la dunia nchini Urusi, ni rafiki wakaribu wa Aubameyang, tangu wawili hao wakiwa wachezaji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Meneja mpya wa Arsenal Unai Emery aliwahi kukiri kuwa shabiki mkubwa wa Dembele, ambaye kwa sasa yupo katika mazingira magumu ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Barca kufuatia kusajiliwa kwa mshambuliaji wa pembeni kutoka Brazil, Malcom.

Wakati Arsenal wakihusishwa na mpango wa kutaka kumsajili Dembele, FC Barcelona nao wanatajwa kuhitaji huduma ya kiungo kutoka Wales na klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London Aaron Ramsey, huku ikiripotiwa huenda pakafanyika biashara ya kubadilishana wachezaji hao, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Dembele alijiunga na FC Barcelona akitokea Dortmund msimu uliopita kwa ada ya Pauni milioni 97.

Usajili wake ulichagizwa na hatua ya kuondoka kwa mshambuliaji wa Brazil Neymar aliyetimkia PSG, lakini mpaka msimu wa 2017/18 unamalizika mwezi Mei, alikua ameshacheza michezo 17 ya ligi ya Hispania, kufuatia majeraha ya nyama za paja yaliyomkabili kwa kipindi kirefu.

Max Meyer anasa kwenye rada ya Crystal Palace
Cristiano Ronaldo kuikabili Real Madrid