Hatmaye mchezaji wa timu ya Arsenal, Mesut Ozil amefunguka kuhusu hatima yake ndani ya club ya hiyo huku akisistiza kuwa amejitoa vya kutosha kwa club yake msimu huu na hajali wanaotoa lawama juu yake.

Mlinzi wa zamani wa Arsenal, Martin Keown hivi karibuni alimtupia lawama kiungo huyo ambaye ndie mchezaji alievunja rekodi ya kununuliwa kwa pesa nyingi zaidi klabuni hapo kuwa hakushirikiana vizuri na wachezaji wenzake katika mchezo dhidi wa mahasimu wao Tottenham mwezi uliopita, ambapo Arsena walichapwa mabao mawili kwa sifuri.

“Nimecheza Real Madrid, nimecheza pia katika timu yangu ya taifa Ujerumani na nimekuwa nikisifiwa nakukosolewa kwa hiyo kukosolewa kunanijenga kuwa vizuri zaidi” amesema Ozil.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 12, 2017
Bob Marley atimiza miaka 36 tangu afariki dunia