Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ujerumani na klabu ya Arsenal Mesut Ozil huenda akaondoka kaskazini mwa jijini London, na kutimkia nchini Uturuki kujiunga na klabu ya Fenerbahce.

Ozil ambaye amekua na wakati mgumu ndani ya kikosi cha Arsenal kufuatia jina lake kuenguliwa kwenye usajili wa Ligi Kuu na Michuano ya kimataifa, anahushishwa na taarifa hizo, huku ikielezwa usajili wake utakamilishwa mwezi Januari 2021.

Taarifa kutoka kwa rafiki wa karibu na kiungo huyo aliejiunga na Arsenal mwaka 2013 akitokea kwa mabingwa wa Hispania Real Madrid Murat Zorlu zinasema, kuna asilimia 90 kwa Ozil kuondoka London.

“Nina uhakika 90% Ozil atakuja Uturuki kwenye dirisha la usajili la Januari, Chanzo kilichopo karibu zaidi na klabu kimenieleza kuwa Ozil anauwezekano mkubwa wa kuwa mchezaji wa Fenerbahce kwenye dirisha la usajili lijalo. Ninaweza kusema 90% atajiunga na sisi mwezi ujao.” Zorlu ameimbia Sport Digitale.

Ozil amekuwa akihusishwa na timu za Uturuki kwa muda sasa, inasemekana ana wafuasi wengi wanaomshabikia nchini Uturuki. Pia, mke wa Ozil alikuwa Miss Uturuki mwaka 2014 na Ozil mwenyewe anaasili ya Uturuki.

Tangu kuondoka kwa Arsene Wenger, Mesut Ozil amekuwa na maisha magumu ndani ya klabu ya Arsenal.

Meneja alieajiriwa baada ya kuodnoka kwa babu huyo kutoka nchini Ufaransa, Unai Emery alishindwa kumtumia kiungo huyo aliekua sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2014, kwenye kikosi cha Arsenal, hali kadhalika kwa meneja wa sasa Mikel Arteta.

Katika msimu wa mwisho wa Arsener Wenger kukinoa kikosi cha Arsenal, Ozil alisaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Arsenal na aliongezewa mshahara na kufikia pauni 350,000 kwa juma, huu ni mshahara mkubwa zaidi ukilinganishwa na mishahara ya wachezaji wengine wote wa klabu hiyo.

Mino Raiola achafua hali ya hewa Old Trafford
Balotelli aibukia Sirie B