Kiungo mshambuliaji wa Arsenal Mesut Ozil anaripotiwa kuwa katika mpango wa kutaka kurejea Santiago Bernabeu yalipo makao makuu ya klabu ya Real Madrid.

Gazeti la The Marca limeeleza kuwa, Ozil yupo tayari kuona jambo hilo linafanikishwa wakati wowote kuanzia mwishoni mwa msimu huu, kutokana na kuamini bado anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Zidane.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 mara kadhaa anadaiwa kuelezea majuto ya kuondoka Real Madrid huku akikiria bado anaihusudu klabu hiyo ambayo inashikilia ubingwa wa barani Ulaya.

Ozil alijiunga na Arsenal mwaka 2013 kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 42.5, na sababu ya kuondoka Santiago Bernabeu ilitajwa kuwa, alihusudu sana starehe na kuweka kando masuala ya soka.

Hali kama hiyo inaripotiwa kwa Angel Di Maria ambaye aliondoka Real Madrid mwaka 2014, kwa sababu za kutoelewana na aliyekua meneja klabuni hapo Carlo Ancelotti.

Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa anawatumikia mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG, inasemekana huchukua muda wake kuelezea maisha ya Real Madrid na wakati mwingine hufika mbali zaidi na kusema ilikua kama bahati mbaya kuondoka klabuni hapo.

West Ham Utd Kumfungia Kazi Payet
Lukuvi ayageukia mabaraza ya ardhi, aonya kukithiri kwa rushwa