Kiungo kutoka nchini Ujerumani Mezut Ozil ameungana na meneja wake Arsene Wenger kwa kuwataka mashabiki wa klabu ya Arsenal kuwa wastahamilivu.

Ozil amepeleka ujumbe huo kwa mashabiki wa The Gunners, kufuatia kichapo cha mabao manne kwa sifuri walichoangshiwa jana na majogoo wa jiji Liverpool, katika mchezo wa mzunguuko wa watatu wa ligi kuu ya soka nchini England.

Kiungo huyo amesema suala la ustahamilivu linapaswa kupewa kipaumbele miongoni mwa mashabiki walioonyesha kuwa na hasira ya kupata matokeo mabaya katika michezo miwiwli mfululizo.

Arsenal ilipoteza mchezo dhidi ya Stoke City kwa kufungwa bao moja kwa sifuri majuma mawili yaliyipita, kabla ya kubanjuliwa na Liverpool hapo  jana.

Katika hatua nyingine Ozil amewataka mashabiki wa The Gunners kuwalaumu wachezaji na sio meneja wao Arsene Wenger, kwa kusema wao ndio walikuwepo uwanjani wakiwajibika na kilichowakuta ni makosa ya kiuchezaji.

“wanapaswa kutulaumu sisi, maana tulikua uwanjani tukicheza na tulikosea, ndio maana tukaadhibiwa na wapinznai wetu”.

“Litakua jambo la kipuuzi endapo lawama zitaelekezwa kwa meneja, najua wapo baadhi ya mashabiki wanamlaumu, lakini ninawataka watulaumu sisi wachezaji ambao ndio tumefanya makosa na kupelekea kufungwa idadi ya mabao manne uwanjani”. Amesema Ozil

Hata hivyo Ozil amewataka radhi mashabiki wa Arsenal kwa matokeo hayo na ameahidi watajirekebisha katika michezo mingine inayofuata.

Arsenal imeendelea kuwa na point tatu ilizozivuna katika mchezo wa kwanza dhidi ya Leicester City waliokubali kichapo cha mabao manne kwa matatu, na kwa sasa inashika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi ya nchini England.

Klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London itarejea tena uwanjani Septemba 09 kucheza dhidi ya AFC Bournemouth, baada ya kupisha wiki ya FIFA.

Zitto: Uhuru wa demokrasia unaminywa nchini
NEC yavitaka vyombo vya habari nchini kuiga mfano wa wenzao Kenya