Jarida la Forbes limetoa orodha ya mastaa waliolipwa pesa nyingi zaidi duniani huku mwanamziki na mfanya biashara Sean John Combs ‘P Diddy’ akiongoza orodha hiyo.

Orodha hiyo ya mastaa 100 imejumuisha watu kutoka tasnia mbali mbali kama vile watangazaji, wanamziki na wana michezo mbali mbali.

Orodha hiyo imejumuisha kipato kilichoingizwa na mastaa husika kutokea juni 1,2016 hadi juni 1,2017.Fedha hizo ni kabla ya makato ya wanasheria mameneja na mawakala wa mastaa hao.

Hapa chini ni orodha ya mastaa 10 walioingiza fedha nyingi zaidi;

  1. Diddy-$130 milioni (Tsh bilioni 291)
  2. Beyonce-$105 milioni (Tsh bilioni 235)
  3. J.K Rowling-$95 milioni (Tsh bilioni 213)
  4. Drake-$95 milioni (Tsh bilioni 210)
  5. Cristiano Ronaldo-$93 milioni (Tsh bilioni 208)
  6. The Weekend-$92 milioni (Tsh bilioni 206)
  7. Howard Stern-$90 milioni (Tsh bilioni 203)
  8. Coldplay-$88 milioni (Tsh bilioni 196)
  9. James Patterson-$87 milioni (Tsh bilioni 195)
  10. Lebron James-$86 milioni (Tsh bilioni 192)
Video: Chin Bees afunguka ya 'Nyonga Nyonga' Awagusa Navy Kenzo na walichomtibua
Usajili Wa Lacazette: Olympic Lyon Yatangaza Masharti

Comments

comments