Mtayarishaji gwiji wa muziki wa kizazi kipya, P-Funk Majani ambaye hivi karibuni alitambulisha rasmi kundi lake jipya la Bongolos amesema jina la wimbo huo lilitolewa na mkali wa ‘This is Why Im Hot’, MIMS.

P-Funk amesema kuwa wazo hilo lilipatikana kupitia wimbo wa ‘You Can Never Be Me’ alioutayarisha yeye ambapo Jay Mo alisikika sambamba na MIMS, miaka mitano iliyopita.

“Tangu tulivyopiga ile ngoma na tukapata vocal za MIMS na Jay Mo akaweka vocal na jamaa mwingine wa Marekani anaitwa Immu Cabir, kwenye verse ya MIMS alichana akasema ‘Welcome to the Jungle, Bongolos… yaani nikasema hili ni jina la kundi, Bongo Records, Bongo Flava,” P- Funk aliiambia Friday Night Live ya East Africa TV.

Alifafanua kuwa maana ya jina hilo ni Uafrika na utafutaji wa watu ambao ni kama wanaishi msituni.

Bongolos inayoundwa na wasanii wawili akiwemo msanii wa kike ‘Tamu’, wameachia wimbo wao wa kwanza waliouita jina la ‘Wape’.

Video: Sirro azungumza kuhusu Askari aliyepiga risasi hewani
Video: Wakazi, P The MC, Zaiid Waifungukia ‘SSK’ na ngoma ya ‘Habari ya Leo’