Mapacha Peter na Paul wako katika mtafaruku mkubwa na kundi lao likiwa katika ukingo wa kusambaratika.

Jana, Peter aliweka hadharani hali ya mgogoro ulio katika kundi hilo akieleza kuwa yeye hana tatizo na Paul lakini ana tatizo na menejimenti ya kundi hilo ambayo inaongozwa na kaka yao Jude Okoye.

Alieleza kuwa hivi sasa anataka kufanya biashara ya muziki na sio biashara ya familia, huku tweet nyingine ikieleza kuwa msanii ndiye anayemuajiri meneja na sio vinginevyo.

TWEET

Hata hivyo, Paul alitofautiana na kila alichokifanya Peter na kumponda kwa uamuzi wa kuweka matatizo yao kwenye mitandao ya kijamii. Alipost picha akiwa na kaka yake Jude Okoye na kueleza kuwa walianzia hapo na watabaki hapo kama familia.

Paul and Jude

Alimponda pia Peter kwa kueleza kuwa hataki biashara ya familia, ahoji kuwa kama hataki familia yeye ni nani tena kwake. Alisema familia itabaki kuwa familia na damu moja kwake.

“This is where I belong and this is where I stand…….you do music in the studio, not in social media, you have family issues, you discuss that in close doors, not in social media ….. Family is family, blood is blood …. If you don’t do family business, then who am I to you?” Aliandika.

Hii ni mara ya pili kundi hilo kuingia katika mgogoro mkubwa, ambapo mwaka 2014 lilinusurika kuvunjika.

Paul aliwahi kudai kuwa yeye ndiye anayeandika nyimbo nyingi zaidi za kundi lao.

Ne-Yo kutumbuiza kwenye Mkoa huu Tanzania, Mei 21
Simba Wapanga Jinsi Ya Kuimaliza Yanga, Kutwaa Ubingwa