Beki wa pembeni wa Manchester City, Pablo Javier Zabaleta Girod anaamini atafanikisha mpango wa kuondoka Etihad Stadium na kujiunga na klabu ya AS Roma.

Beki huyo kutoka nchini Argentina amepanga kuondoka Etihad Stadium, kufuatia kutokuwa sehemu ya mipango ya meneja mpya wa Man City, Pep Guardiola.

Zabaleta, amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja na Guardiola ameagiza mchezaji huyo asisainishwe mkataba mpya, hali ambayo inatoa nafasi ya kuondoka.

Tayari kiasi cha Pauni milion 2.5, kimeshatajwa kama ada ya uhamisho wa beki huyo mwenye umri wa miaka 31.

Zabaleta alijiunga na klabu ya Man City mwaka 2008, akitokea nchini Hispania alipokua akiitumikia klabu ya Espanyol, na mpaka sasa anajipanga kuondoka mjini Manchester amefanikiwa kucheza michezo 198 na kufunga mabao 7.

Sarakasi Za Uongozi Wa Stand Utd Zaendelea
Real Madrid Wapanga Kuitega Juventus