Timu ya Bingwa wa Masumbwi wa Shirikisho la Ngumi Duniani (WBA) uzito wa ‘Welterweight’ Lucas Matthysse imeahidi kumzimisha Manny Pacquiao kabla ya kengele ya mwisho, katika pambano la Julai 15 mwaka huu nchini Malaysia.

Matthyse atapigana na Pacquiao katika jiji la Kuala Lumpur ikiwa ni mwaka mmoja tangu bondia huyo wa ufilipino apoteze ubingwa wake alipokutana na Jeff Horn nchini Australia.

Meneja wa Matthysse anayefahamika kama Arano Mario alisema kuwa wana uhakika wa kumpumzisha kabisa Pacquio kwakuwa muda wake umekwisha.

“Bado nafikiri tutampiga Pacquiao kwa KO, muda wake umekwisha, inabidi apumzike,” alisema Mario.

“Tangu miaka mitatu iliyopita tulitaka pambano na Pacquiao. Kila mtu anajua kuwa hili ni pambano ambalo tulikuwa tunalisubiri kwa hamu na tuna uhakika wa kumpiga,” aliongeza.

Kwa upande wa Matthysse ambaye pia anaamini atamzimisha bondia huyo machachari kutoka Ufilipino, alisema kuwa atampa nafasi Pacquiao ya pambano la marudiano baada ya kumpiga.

Pacquiao amerejea kwenye mapambano akiwa na nia ya kuwezesha pambano lijalo linalosubiriwa kwa hamu zaidi kati yake na bondia machachari, Vasyl Lomachenko.

Zoezi la usambazaji gesi majumbani kuanza rasmi leo
Polisi wahaha kumsaka paka uwanja wa ndege

Comments

comments