Bingwa wa dunia wa masumbwi uzito wa welterweight wa Shirikisho la Masumbwi Duniani (WBO) amesema kuwa hatajisumbua kuangalia pambano linalovuta usikivu wa mamilioni ya watu, kati ya Floyd Mayweather na Conor McGregor.

Pacquiao ambaye yuko nchini Australia akijiandaa na pambano kati yake na bingwa masumbwi asiyepigika nchini humo, Jeff Horn amesema kuwa hataliangalia pambano hilo kwa sababu halitakuwa na mvuto hata kidogo.

“McGregory hana nafasi yoyote kwenye hili pambano,” alisema Pacquiao. “Nadhani litakuwa linaboa sana, hakuna namna ambayo ataweza kufikisha sumbwi lolote la maana kwa Mayweather, sasa atawezaje?” alihoji Seneta huyo wa Ufilipino.

Alisema kutokana na sababu hizo, hatashuhudia pambano hilo lakini analisubiri pambano kati ya Gennady Golovkin na Canelo Alvarez litakalofanyika Septemba 16, akidai litakuwa pambano halisi.

“Pambano halisi ni kati ya Golovkin na Canelo. Ni pambano kali kwa sababu bondia bora anapambana na bondia bora, hilo ndilo pambano nitakaloangalia,” aliiambia Yahoo Sports.

Alichokisema Pacquiao kinaungwa mkono na baadhi ya wadau  wa masumbwi ambao wanajaribu kulinganisha namna ambavyo Mfilipino huyo alivyoweza kufikisha ngumi za maana 81 tu kwenye mwili wa Mayweather kwenye pambano lao la mwaka 2015, ingawa anasifika kwa kasi na uzito wa ngumi.

Hivyo, kuna ugumu zaidi kwa Mcgregor ambaye hanajawahi kushiriki mchezo wa masumbwi ingawa ni bingwa wa mchezo wa ngumi, mateke (UFC).

Mayweather na McGregor wanatarajia kukata mzizi wa fitna Agosti 26 mwaka huu, Las Vegas Marekani.

Gambo awapiga dongo wapinzani, asema kama hawatabadilika watapotea
Wachezaji wa kimataifa waweka historia Mlima Kilimanjaro