Hatimaye bondia Mfilipino, Manny Pacquiao ametimiza ndoto yake ya kuwa Seneta wa kwanza duniani anayeshikilia mkanda wa ubingwa wa dunia wa WBO uzito wa ‘Welterweight’ baada ya kumchapa Jessie Vargas.

Pacquiao (59-6-2) ametangazwa kuwa mshindi wa pambano hilo lilifanyika alfajiri ya leo (kwa majira ya Afrika Mashariki), Vegas nchini Marekani, baada ya kukamilika kwa raundi 12 akimpiga chini Vargas (27-2-0) mara tatu lakini refa wa pambano hilo alihesabu moja kati ya hizo na nyingine ziliamliwa kuwa zilitokana na kuteleza.

pacquiao-wbo

Manny Pacquiao akiwa na mkanda wa ubingwa wa WBO, kushoto ni Mkufunzi wake, Freddie Roach  pamoja na timu yake

Kwa mujibu wa waamuzi watatu wa pambano hilo, Pacquiao alishinda kwa 114-113, 118-109 na 118-109. Matokeo ya jaji wa kwanza yanayoonesha ushindi mwembamba yamekosolewa vikali na mtandao wa Telegram ambao umedai kuwa Pacquiao alipata ushindi wa wazi kwa raundi zote sita za mwisho pamoja na raundi tatu za awali.

Pacquiao mwenye umri wa miaka 37 alianza kumchanganyanya Vargas ambaye ni kijana mwenye umri wa miaka 27 aliyekuwa akitetea ubingwa wake, alipompiga chini katika raundi ya pili ya pambano hilo.

manny-pac-na-vargas

Akizungumza baada ya kumalizika kwa pambano hilo, Pacquiao alisema kuwa anajisikia furaha na kwamba anatarajia kupanda tena ulingoni.

“Sijui nitapigana na nani, nitapiga na mtu yoyote na promota wangu anataka nipigane. Yeyote kwenye uzito wa kilo 67 (147 lbs),” alisema Pacquiao.

Pacquiao amekuwa akiota kuwepo kwa mpambano wa marudiano kati yake na Bingwa ambaye hajawahi kushindwa, Floyd Mayweather. Hata hivyo, Mayweather alitangaza kustaafu japo watu wake wa karibu wanadai ameanza kujifua taratibu.

Naye Vargas alipoulizwa kuhusu hali ya pambano hilo, alisema lilikuwa na ushindani wa karibu na kwamba kilichomchanganya mwanzoni ni kasi ya Pacquiao iliyompeleka chini.

“Nadhani lilikuwa ni pambano la ushindani wa karibu. Pambano la kukimbizana. Tulikubanana wote! Kasi yake ilinishangaza mwanzoni,” alisema Vargas.

“Ninawaomba radhi mashabiki kwa kuwaangusha, lakini nilijitahidi kadiri ya uwezo wangu na tunazidi kuwa bora. Kupigana na Pacquiao tu kumeinua mchezo wangu na inanifanya kuwa bora zaidi,” aliongeza.

Mwanaume mwenye bunduki azua taharuki nje ya Ikulu ya Marekani
Video: Trump aondolewa ghafla jukwaani kwa tishio la kupigwa risasi