Padri wa Kanisa Katoliki, Dk Bernard Msike ambaye aliwafungisha ndoa staa wa Hip Hop, Bonaventure Kabogo ‘Stamina’ na mkewe Veronica Peter katika Kanisa la Mt. Maria Consolata mkoani Morogoro, amewaita wanandoa hao kanisani kwa ajili ya usuluhishi.

Padri huyo aliwafungisha ndoa hiyo Mei, 2018 ambayo imedumu kwa takriban mwaka mmoja na miezi kadhaa kisha kumwagana na kuzua gumzo kama lote mitandaoni wiki iliyopita

Akizungumza hayo kufuatia sakata lao kutikisa mitandaoni, padri alianza kwa kusema anasikitika kuona ndoa hiyo imedumu kwa muda mfupi kwani si kawaida yake kufungisha ndoa na kisha kuvunjika.

“Hii nafikiri itakuwa ndoa ya kwanza au ya pili kwa kweli, imenishtua kwa sababu sikutegemea kama wanaweza kuachana ndani ya muda mfupi namna hii,” alisema.

Padri huyo alisema atawaita wawili hao kanisani kwa ajili ya usuluhishi kwani kanisa bado linaitambua ndoa yao.

“Niwaase tu katika kipindi hiki wasije wakaanzisha mahusiano mapya maana watakuwa wanatenda dhambi. Kanisa Katoliki linaitambua ndoa ya mwanaume na mwanamke mmoja tu mpaka kifo kitakapowatenganisha,” alisema.

Stamina na mkewe wameachana na mkali huyo kutoa wimbo wa Asiwaze ambao unatajwa kuwa amemsema mkewe huyo. Sababu kubwa inayotajwa katika kuachana kwa wawili hao ni usaliti.

Chanzo GlobalPublisher

Mtoto wa miaka 10 asakwa na polisi kwa mauaji kisa wivu wa mapenzi
Watu 1000 waachwa bila makazi Dodoma