Mtu mmoja nchini Taiwan amepigwa faini baada ya kumsafirisha paka wake kama kifurushi kwa njia ya mawasiliano ya posta.

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa UDN mtu huyo mwenye umri wa miaka 33 aliyetambulika kwa jina la Yang amepigwa faini ya fedha za Taiwan NT$60,000 ( sawa na dola za Marekani 1,952) kwa kuvunja sheria ya Ulinzi wa Wanyama ya Taiwan.

Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita ambapo, Yang alimfungasha kwenye kifurushi paka wake aina ya Scottish fold na kumpeleka kwenye kituo kimoja cha kuhifadhi wanyama nchini humo katika wilaya ya Banciao, ambapo amesema kuwa hakuwa anahitaji tena kuendelea kumfuga Paka huyo.

Aidha, kutokana na kosa hilo, alipigwa faini ya ziada ya NT$30,000 kwa kuvunja sheria ya kuzuia na kupambana na magonjwa ya kuambukiza ya wanyama sababu wafanyakazi wa kituo cha wanyama alipopokelewa Paka huyo waligundua kuwa hakupewa chanjo ya kichaa na kuzuia hasira kali.

Maafisa wa ulinzi wa wanyama jijini Taipei walifanikiwa kumnasa mtuma kifurushi hicho kupitia kampuni ya posta na mkanda wa kamera za ulinzi za polisi

Kwa upande wake, mkurugenzi wa mamlaka ya wanyama, Chen Yuan-chuan, amelaani vikali tukio hilo, huku akisema Mnyama anaweza kupatwa na hali mbaya kwa kukosa hewa ndani ya kifurushi na kupandwa na ghadhabu pia hakukuwa na maji safi na salama.

Hata hivyo, Yuan-chuan amewataka watu kufuata taratibu halali za kisheria pale wanapoona hawawezi tena kuendelea kuwatunza wanyama wao wa nyumbani.

Mahakama yapiga chini shauri la kupinga Muswada wa Vyama vya Siasa
Mzimu uliomng’oa Mugabe waanza kumvuta Mnangagwa