Paka aliyekuwa akimilikiwa na mkongwe wa mitindo Duniani marehemu, Karl Lagerfeld ndiye atakayerithi utajiri wote wa mkongwe huyo.

Paka huyo anayefahamika kwa jina la Choupette atamiliki utajiri wake ambao unatajwa kufikia zaidi ya shilingi Bilioni 456 za Kitanzania na inaripotiwa kuwa paka huyo alikuwa akilelewa kifahari na mmiliki wake tangu mwaka 2011.

Karl Lagerfeld alifariki Jumanne ya  Februari 19, 2019 jijini Paris akiwa na umri wa miaka 85 akiwa miongoni mwa watu ambao walikuwa nyuma ya pazia ya mafanikio ya nembo kama Tommy Hilfiger, Chanel na Fendi mwaka 1980.

Hata hivyo, umaarufu wa paka huyo umekuwa mkubwa hata katika mitandao ya kijamii, ambapo katika ukurasa wake wa Instagram unaoendeshwa na mtaalam wa masoko mitandaoni, Ashley Tschudin, umefikisha jumla ya wafuasi 120,000.

Majaliwa awataka viongozi CCM kutekeleza majukumu yao
Mkuchika kuchukua hatua kali dhidi ya watumishi wa umma

Comments

comments