Hivi karibuni Mr T Touch ambaye ni producer wa Free Nation amekuwa akitumiwa na wasanii wengi na pia miongoni mwa watayarishaji wanaokubalika zaidi kwa sasa.

anajulikana kwa kutengeneza hits kali za Ney wa mitego, bill nas na wengine kibao lakini safari hii amepata ugeni mwingine kutoka kwa bi dada Pamela ‘Pam D’

Nyimbo karibu zote zilizomtambulisha Pam D nchini zikiwemo Nimempata na Popo Lipopo zimetayarishwa na Mesen Selekta, na sasa anataka kubadilisha ladha.

13473345_621726737981116_1929501875_n

Akiongea na kipindi cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka, Pam amesema wimbo wake mpya Nipe Nono aliomshirikisha Nay wa Mitego umetayarishwa na Mr T Touch.

“Nilitaka watu waone kuna utofauti sio kila siku Mesen tu mwisho wa siku watu watakuwa wanasema Pam bana anabebwa na Mesen kwahiyo ilinibidi niamue kufanya katika studio nyingine,” alisema.

Wimbo huo utatoka Ijumaa hii.

 

 

Jose Mourinho Aichokonoa Arsenal
Argentina vs Chile Fainali Copa America