Kikosi cha Pamba FC kipo jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Mabingwa Watetezi Simba SC.

Pamba FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza itakua mgeni wa Simba SC kesho Jumamosi (Mei 14) saa moja usiku, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa Pamba FC Moses William amesema kikosi chao kipo tayari kwa mchezo huo, japo wanaiheshimu Simba SC ambayo ndio bingwa mtetezi wa michuano ya ‘ASFC’.

Moses amesema Morari ya wachezaji wao juu sana, na wanaamini hatua hiyo itaweza kuwavusha na kutinga Nusu Fainali ya ‘ASFC’ kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu yao yenye maskani yake makuu jijini Mwanza.

“Dhamira yetu ni kupambana na kupata ushindi dhidi ya wapinzani wetu, tunawaheshimu sana kwa sababu mchezo wa soka unashurutisha heshima kwa mpinzani, lakini hatuwahofii kwa sababu tunakwenda kupambana tukiamini wao watacheza soka kama ilivyo upande wetu.”

“Uongozi wa Pamba FC umefanya kazi kubwa sana ya kuongea na wachezaji ili kufanikisha lengo la kuifunga Simba SC na kusonga mbele kwenye michuano hii, tunaamini hili linawezekana na wachezaji wametuhakikishia.”

“Nina msemo wangu ambao ninapenda kuutumia ‘Haukatazwi Kushindana Lakini Usimchukie Mshindi’ kwa hiyo sisi tunakwenda kwenye mchezo dhidi ya Simba SC, kwa sababu ni hatua ya mtoano lazima kuna timu moja itafuzu kwenda hatua inayofuata, ikitokea wo wamefuzu haituzuii sisi kutengeneza Plan yetu kuelekea kwenye mchezo.”

Katika hatua nyingine Moses amesema hawaihofii Simba SC kwa sababu kama ukubwa hata Pamba FC ni kubwa na ina historia katika Soka la Bongo.

“Ukiondoa Simba na Young Africans zenye mashabiki wengi nchi hii, Pamba FC nayo ni miongoni mwa timu zenye mashabiki na historia kubwa nchi hii, kwa nini tuogope kwenda kucheza mchezo dhidi yao?” ameohiji Moses William

Mshindi wa mchezo wa kesho Jumamosi (Mei 14) atacheza hatua ya Nusu Fainali dhidi ya Young Africans iliyotangulia kwenye hatua hiyo kwa kuibamiza Geita Gold kwa changamoto ya Mikwaju ya Penati.

Uongozi Pamba FC wafunguka, watoa ahadi kwa wachezaji
Biashara United Mara kurudi nyumbani Musoma