Kufuatia kifo cha Mtayarishaji wa muziki nchini, Pancho Latino aliyefariki dunia jana Oktoba 9, 2018 katika kisiwa cha Mbudya jijini Dar es salaam ambaye kwa sasa mwili wake upo hospitali ya Lugalo kusubiri ratiba za mazishi zikiwa zinaandaliwa na watu wake wa karibu kwa kushirikiana na familia yake.

Kwa mujibu wa mpiga picha maarufu, MxCarter ambaye ni moja ya watu wa karibu wa marehemu amesema enzi za uhai wa Pancho amewahi kuzungumza kuwa hataki siku ya mazishi yake vyombo vya habari kufaidika na kufanya msiba huo kuwa kitu kikubwa, amewahi kusema hataki kuagwa Leaders Club kama ambavyo mazishi ya wasanii wengine yamekuwa yakifanyika na kusema mwili wake urudishwe nyumbani kwao Morogoro huko Gairo.

Hivyo kwa mujibu wa maneno hayo ambayo marehemu amekuwa akiyazungumza enzi za uhai wake, kamati ndogo iliyokaa kujadili mazishi yake imeridhia kufanya hivyo.

”Kwahiyo hakutakuwa na hiyo ishu ya Leaders, na kutakuwa na taratibu za kawaida kama mtu wa kawaida anayeenda kupumzishwa nyumba yake ya milele” amesema MxCarter.

MxCarter amesema kuwa Pancho alikuwa Mbudya kwa ajili ya mkutano wa kibiashara na Wajerumani waliotaka kufanya naye kazi za muziki lakini mara baada ya kikao hiko Pancho alienda kuogelea ambapo maji yalivumta.

”Alifika kule na katika kujaribu kutaka kuogelea nafikiri na kutokujua maji ni mengi au ni nini , yalimvuta yale maji kwa mujibu wa watu waliokuwa kule na gafla walimuoana nafloat (elea) na wakajaribu kumsaidia lakini Mungu alionesha upendo zaidi kwa Pancho.

Mungu aipumzishe roho ya marehemu Pancho kwa amani.

 

Nafasi 10 za ajira kutoka makampuni 10 Tanzania
Video: Usikanyage 'BEACH' hizi, chukua tahadhari ni hatari kwa maisha yako,