Siku chache baada ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuwasimamisha Wakugurenzi wake Sita, Mameneja watano na Mhasibu Mkuu, shirika hilo limetangaza kusitisha mishahara ya wafanyakazi wake walioshindwa kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma zao.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa kutokana na baadhi ya wafanyakazi hao kushindwa kuwasilisha vyeti hivyo kama walivyoagizwa kufanya hivyo kabla ya Juni 24 mwaka huu.

Alisema kutokana na hali hiyo, Shirika hilo halitawalipa mishahara wafanyakazi hao hadi watakapowasilisha vyeti vyao kwa Wakuu wa idara na Mameneja wa Kanda kama agizo la Serikali lilivyowataka.

“Nawajulisha kuwa wote walioshindwa kuwasilisha vyeti hawatalipwa mishahara yao hadi watakapowasilisha vyeti hivyo kama ilivyoelekezwa,” alisema Mkurugenzi Mkuu huyo katika barua yake kwa wakuu wa idara za ofisi hiyo.

Agizo hilo linatokana na maagizo ya Serikali ya kufanya uhakiki na kuwabaini wafanyakazi hewa na wasio na vigezo vya kuwa katika nafasi mbalimbali za utumishi wa umma.

Mipango Ya Jurgen Klopp Kumuondoa Joe Allen Anfield
Man Utd Waingia Kwenye Mtego Wa Juventus FC