Vijana wenye umri mdogo wanaofanya uhalifu kwenye kata mbalimbali za wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera waonekana kuwa tishio kwa wananchi kutokana na kukithiri wa vitendo hivyo huku hatua zikiwa hazichukuliwi.

Miongoni mwa madiwani waliojadili hojaa hiyo ni diwani wa kata ya Kalenge, Erick Method, wakati akiwasilisha taarifa ya kata yake  kwenye Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo lililofanyika Mei 10, mwaka huu, ambapo amesema licha ya jitihada za wananchi kuwakamata watoto hao jeshi la polisi limeshindwa kuwafikisha mahakamani kwa madai kuwa wana umri chini ya miaka 18.

Awali akitoa elimu ya ulinzi shirikishi kwa madiwani, watendaji wa kata, vijiji, wenye viti wa vijiji na vitongoji, kamishna wa ushirikishwaji jamii polisi makao makuu, Dk. Mussa Ali Mussa, amesema uharifu hauwezi kwisha nchini iwapo jamii haitakuwa tayari kushirikiana na jeshi la polisi.

Amesema uhalifu umekuwa ukitamalaki kwenye jamii kutokana na kamati za ulinzi na usalama ngazi ya kata kushindwa kutimiza wajibu wao na kwamba kuna kila sababu kwa   kutenga bajeti kwaajili ya ulinzi na usalama badala la kujikita kwenye miradi ya maendeleo pekee.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka madiwani kuwahamasisha wananchi na wafanyabiashara kuchangia miradi ya polisi ikiwemo ujenzi wa vituo vya polisi kwa lengo la kudhibiti uharifu kabla na baada ya kutokea.

Licha ya kupongeza mpango wa polisi kata, Diwani wa kata ya Biharamulo mjini, David Mwenenkundwa, amedai uwepo wa askari hao utasaidia kupunguza matukio ya kiharifu na kwamba utaongeza mahusiano ya kuoana na kuoleana.

Wabunge wanawake waliovuliwa uanachama CHADEMA wahudhuria Baraza kuu
Mwandishi wa Al Jazeera auwawa kwa Risasi kichwani