Wakulima wa Kata ya Kiberege Wilayani Kilombero mkoani Morogoro, wamejikuta katika wakati mgum baada ya mazao yao kuvamiwa na panya waharibifu, na kusababisha uharibifu mkubwa katika  mazao ya mpunga na mahindi ambayo wameyapanda katika msimu huu.

Wakulima wa kata hiyo wamesema tatizo hilo limeanza kwa muda mrefu, na cha kushangaza licha ya mvua kunyesha bado panya hao wameendelea na uharibifu, hali ambayo inawapa mashaka juu ya hali ya chakula itakavyokuwa msimu huu.

Aidha wakulima hao kutoka katika vijiji vya Nyamwezi na Misufini, wamedai kuwa ndiyo  mara ya kwanza kuwanaona panya hao wakiharibu mazao yao.

Hata hivyo, kwa upande wake Afisa Kilimo wa Kata ya Kiberege amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na ameeleza kuwa Serikali ya Wilaya hiyo imeanza kuchukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha inakabiliana na tatizo hilo

 

 

Video: Mzee Kingunge alirejea Katoliki kabla ya mauti, Chadema wajitosa majaji wala 'bata'
Yalivyoandikwa magazeti ya nje na ndani ya Tanzania leo