Aliyekua nahodha wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya AC Milan Paolo Maldini, ameanza vibaya katika michuano ya kimataifa ya Tennis, kwa kuondolewa kwenye michuano ya Aspria Tennis Cup mjini Milan.

Maldini ambaye anaunda timu moja na Stefano Landonio, amepoteza mchezo huo kwa kufungwa na Tomasz Bednarek na Dutchman David Pel wote kutoka Poland.

Gwiji huyo wa soka ambaye atatimiza umri wa miaka 49 siku ya jumatatu, na Landonio mwenye umri wa miaka 46, wanashika nafasi ya 975 duniani. Wamekubali kupoteza mchezo wao kwa kufungwa seti mbili kwa sifuri ambazo ni 6-1 na 6-1.

Hata hivyo mchezo huo ulichukua muda wa dakika 42, hadi mshindi alipopatikana, hali ambayo inadhihirisha Maldini na mwenzake walipambana kwa muda mrefu.

Maldini alifaulu kucheza michuano ya kimataifa ya Tennis, majuma mawili yaliyopita baada ya kufanya vyema katika michezo ya ngazi za chini ya mchezo huo maarufu duniani.

Diego Simeone Amuweka Kiporo Zlatan Ibrahimovic
Valere Germain Apata Kiota Kipya Ufaransa