Aliyekua beki na nahodha wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya AC Milan Paolo Maldini, amegeukia mchezo wa Tennis, baada ya kutundika daruga mwaka 2009.

Gwiji huyo anaeendelea kukumbukwa katika medani ya soka nchini Italia, amekua mdau mkubwa wa mchezo wa Tennis, na sasa imedhihirika alikua na kipaji kingine cha kuutumikia mchezo huo.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Maldini ameweka picha inayoonyesha akiwa na tuzo huku akiandika “Nipo Tayari kwa michuano ya kimataifa ya Tennis (ATP).”

Mwishoni mwa juma lililopita, alimshinda mpinzani wake  Stefano Landonio katika mchezo wa kumpandisha kiwango na kuingia kwenye michuano ya kimataifa ya Tennis.

Ready for the Aspria Milano ATP Challenger ???

A post shared by Paolo Maldini official (@paolomaldini) on

Kuhusu umri, Maldini amesema kuwa na umri wa miaka 48 sio tatizo kubwa sana kwake, zaidi ya kutambua anakwenda kuwa mmoja wa watu watakaoonyesha uwezo kwenye michuano ya kimataifa ya Tennis (ATP).

Kwa sifa aliyofikia Maldini atakuwa na nafasi ya kushiriki michuano ya wazi ya Austrlian, Wimbledon, French na USA.

Akiwa katika viwanja vya soka, Maldini alicheza michezo 600 akiwa na klabu ya AC Milan, na kwa upande wa timu ya taifa ya Italia alicheza michezo 126.

Familia ya Ndesamburo yakanusha kuwepo mgogoro kati yake na Chadema
Vigogo wa IPTL wapandishwa kizimbani