Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis  amelazimika kuendesha ibada ya Jumapili ya Pasaka kwa njia ya mtandao badala ya kukaa na waumini kutokana na khofu ya kirusi cha corona.

Akiendesha ibada hiyo siku ya Jumapili leo, ambayo mtu pekee aliyekuwa mbele yake alikuwa mpigapicha wake, Papa Francis alitoa wito kwa walimwengu kutokukubali kutawaliwa na hofu katika wakati huu dunia inapopambana na ugonjwa wa COVID-19, na badala yake watambuwe kuwa “giza na mauti sivyo vyenye kauli ya mwisho.”

“Kwa wiki kadha sasa, tumeendelea kurejelea kauli kwama ‘mambo yatakaa sawa,’ tukijiambatanisha kwenye uzuri wa ubinaadamu na kuruhusu maneno ya kutia moyo kusimama kwenye nyoyo zetu” Amesema Papa.

Mwaka Jana Misa ya Jumapili ya Pasaka na kile ilihuhudhuriwa na watu 70,000 kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro. Lakini kwa sasa lango la kuingilia makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican, limefungwa na linalindwa na polisi wenye silaha waliovalia vifaa vya kujikinga na maambukizi ya corona.

Ibada hiyo inayowajumuisha pamoja waumini bilioni 1.3 wa Kanisa hilo ulimwenguni inawakilisha kufufuka kwa Yesu Kristo, ambapo waumini mjini Rome walijaza keki mashuhuri za Pasaka siku kadhaa kabla, kuadhimisha sikukuu yao muhimu.

Video: Mkapa, Kikwete wajitosa kuomba mabilioni
Jinsi mgonjwa wa pumu anavyoweza kukabili Corona