Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amelaaniunyama wa kikatili unaofunika ubinadamu kwa aibu na matukio ya umwagaji damu mashariki mwa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC.

Papa ambaye yupo katika ziara nchini humo, amesema amekerwa na unyonyaji wa umwagaji damu unaofanywa na matajiri wa nchi zinazoendelea pamoja na majaribio ya kuigawanya kwa lengo la kuweza kuitawala.

Papa Francis na Rais Felix Tshisekedi.

Katika Ibada hiyo, inakadiriwa kuwa watu wapatao milioni walikusanyika katika eneo la wazi kwa ajili ya kusikiliza hotuba yake eneo la uwanja wa ndege wa N’dole, ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya yake barani Afrika.

Karibu nusu ya idadi ya watu wa Jamhuri ya demokrasia ya Congo ni wakatoliki wengi zaidi ndani ya barala Afrika ana Papa amefika nchini humo ikiwa ni zaidi ya miaka 37 tangu papa John Paul kufanya ziara katika taifa hilo lenye utajiri wa madini na migogoro.

Raphael Varane aiacha Ufaransa, awaita vijana
Biashara ya Kaboni kuineemesha Tanzania: Jafo