Papa Francis, amewataka Raia na Viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini kufungua ukurasa na kutengeneza njia mpya za upatanisho, amani na maendeleo.

Papa ametoa ujumbe huo, katika siku ambayo alitakiwa kuwa ameanza safari ya ziara yake ya wiki moja katika nchi hizo mbili za Afrika.

Hata hivyo, alilazimika kukatisha safari yake kwa nchi hizo kutokana na sababu ya maumivu ya goti ambayo yamemfanya kushindwa kutembea na kusimama.

Katika ujumbe huo, papa amesema “nimesikitishwa sana na mabadiliko ya ziara yake na kuahidi kutembelea katika nchi hizo haraka iwezekanavyo.”

Mabango yaliykuwa yaimkaribisha Papa Fransis nchini DRC yakiwa yametundikwa barabarani katika mji wa Goma uliopo mashariki mwa nchi hiyo.

Aidha, amewataka wananchi wa nchi zote mbili kutokubali kuporwa matumaini, licha ya vurugu, misukosuko ya kisiasa, unyonyaji na umaskini ambao alisema umewaumiza kwa muda mrefu.

“Mna dhamira kubwa, ninyi nyote, kuanzia viongozi wenu wa kisiasa na dhamira yenyewe ni ile ya kufungua ukurasa mpya ili kupata njia za upatanisho na msamaha, na kuweza kuishi kwa utulivu na kupata maendeleo,” amesema Papa Francis.

Ingawa hakuweza kusafiri, lakini anatarajiwa kuadhimisha misa maalum katika Kanisa la Mtakatifu Petro siku ya Jumapili kwa jumuiya ya waroma wa Wakongo.

Msaidizi wake Kadinali Pietro Parolin, tayari ameagizwa kutembelea nchi za Kongo na Sudan Kusini wiki hii katika siku ambazo Papa mwnyewe alipaswa kuwa huko.

Kuahirishwa kwa ziara ya Papa kulileta mfadhaiko kwa wakazi wa DRC, ambao walikuwa na matumaini ya kusikiliza kile ambacho waliamini angekisema huenda kingeleta upatanisho mpya kuondoa hali ya mashaka ambayo wameishii nayo kwa muda mrefu.

Mchungaji awateka nyara waumini 'awalamba kisogo' ni unyakuo
Saba wafariki katika ajali Dodoma