Imetaarifiwa kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis amelazwa Hospitali kutokana na maambukizi ya maradhi ya mapafu, baada ya kukabiliwa na matatizo ya kupumua na atakaa hospitali kwa siku kadhaa za matibabu.

Taarifa ya Msemaji wa Vatican, Matteo Bruni imeeleza kuwa Papa mwenye umri wa miaka 86 japo amelazwa kwa maambukizi ya mapafu, lakini hana maradhi ya Uviko – 19.

Hii ni mara ya kwanza kwa Francis kulazwa hospitali tangu alipokaa siku 10 kwenye Hospitali ya Gemelli Julai, 2021 na kufanyiwa upasuaji wa tumbo.

Hata hivyo, kumekuwa na maswali kadhaa kuhusu hali ya afya ya Francis, na uwezo wake kusherekea matukio mengi ya wiki takatifu ambayo inaanza hapo kesho Machi 31, 2023 na Jumapili ya matawi ya Machi 3, 2023.

Kocha The Cranes aitabiria makubwa Taifa Stars
Azam FC yahamishia nguvu ASFC