Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema chuki dhidi ya wageni barani Ulaya inayochochewa na siasa za kizalendo inakumbusha enzi ya Adolf Hitler katika miaka ya1930.

Amesema hayo akiwa na waandishi wa habari wakati akiwa njiani kurejea nyumbani, baada ya kumaliza ziara yake ya barani Afrika.

Papa Francis ameeleza kuwa maradhi hayo yanatumiwa kama sababu ya kujihami dhidi ya wageni wanaoonekana kuchafua damu ya taifa amesema kuwa chuki dhidi ya wageni ni maradhi kama ya surua.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa wakatoliki amesema kuwa inavyoelekea mtindo huo upo barani Ulaya na pia tatizo hilo lipo barani Afrika.

Aidha Papa Francis ametoa wito kwa bara la Ulaya kujifunza kutokana na historia ya karne ya 20, amekumbusha pia juu ya watu wa Ulaya waliohamia bara la Amerika na maafa yaliyosababishwa na mafashisti.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 12, 2019
Video: Mwakyembe aitabilia mema Taifa Stars 'itafuzu kombe la Dunia'