Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa John Francis amewasili nchini Ireland akiwa na huzuni kubwa baada ya Kanisa hilo kushindwa kushughulikia tatizo la unyanyasaji wa kingono wa watoto unaofanywa na mapadri.

Akiwa katika Kasri la Dublin, Papa Francis amesema kuwa anahisi maumivu na aibu kubwa juu ya kushindwa kwa mamlaka ya Kanisa Katoliki kushughulikia kashfa hiyo ya kunyanyaswa kingono watoto.

“Kushindwa kwa mamlaka ya kanisa maaskofu, wakuu wa kidini, makuhani na wengine kushughulikia uhalifu kumesababisha hasira na bado ni chanzo cha maumivu na aibu kwa jumuiya ya Kikatoliki,”amesema Papa Francis

Aidha, Papa Francis atakutana na wahanga wa unyanyasaji wa kingono unaofanywa na Mapadri wa Kanisa Katoliki, wakati wa ziara yake ya masaa 36 nchini Ireland, ambapo ni mara yake ya kwanza katika kipindi cha miongo minne kwa papa wa Kanisa Katoliki kutembelea, Ireland.

Hata hivyo, Mamlaka ya Vatican imesema kuwa ziara hiyo itatoa fursa nyingi za kuweza kulijadili tatizo la unyanyasaji wa kingono linaloendelea katika kanisa Katoliki.

Marekani yatuma Manowari ya kivita kuidhibiti Urusi na China
NEC yaviasa vyama vya siasa kufuata sheria za uchaguzi