Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema kuwa mchezji wa Barcelona, Lionel Messi sio Mungu na anashangaa kwanini baadhi ya watu wanamuita hivyo.

Kauli hiyo ya Papa imekuja baada ya mashabiki wengi kudai kuwa Messi ni Mungu kwenye ulimwengu wa mpira, jina ambalo lilianza kukuzwa hususan nchini kwao Argentina.

Papa Francis amesema kuwa kufanya hivyo ni kumkosea Mwenyezi Mungu na kuvunja amri ya tatu ya Mungu, bila kujali wana maanisha nini.

“Huwezi kusema hivyo, na mimi siamini hivyo. Najua watu wanasema ‘yeye ni Mungu’ wakiwa na maana kuwa ‘tunampenda sana’. Unapaswa kumpenda zaidi Mungu. Ni mtazamo watu wanasema, ‘huu ni muungu kwenye mpira’,”

“Ni namna maarufu ambayo watu wanaitumia kuonesha jinsi wanavyomkubali. Kwa hakika inafurahisha kumuona akicheza. Lakini yeye sio Mungu,” Dailymail wanamkariri Papa Francis, Aprili 2, 2019.

Papa na Messi walikutana mwaka 2013, timu ya Taifa ya Argentina ilipokutana rasmi na kiongozi huyo wa dini huko Vatican. Messi aliongoza timu hiyo kama nahodha na walifanya mazungumzo mafupi na Papa Francis.

Messi ambaye ni mshindi mara tano wa Ballon d’Or, amefanikiwa kiasi kikubwa kwenye ulimwengu wa soka, akifunga magoli 31 katika michezo 27 ya Ligi.

Kamati ya Bunge ilivyomalizana na Lema leo, kusuka au kunyoa kesho
Video: Meya wa jiji la Dar atoa msaada wa Kompyuta