Paraguay imefungua ubalozi wake nchini Israel katika mji mkuu Jerusalem na kuifanya kuwa nchi ya tatu kuhamisha ubalozi wake Tel Aviv katika hatua hiyo ya kisiasa inayoweza kuibua hisia kali.

Rais wa Paraguay, Horacio Cartes, na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu walihudhuria sherehe hiyo ya ufunguzi wa ubalozi huo, huku viongozi wa Palestina wakiyatolea wito mataifa ulimwenguni kuiwekea vikwazo Paraguay.

“Hafla hii ina maana kubwa sana kwa sababu inawakilisha urafiki wa dhati kabisa na uungaji mkono wa Paraguay kwa Israel, upendo nilionao kwa taifa hili muhimu na jasiri umejengwa kwa misingi ya maadili na misimamo ambayo inalingana na yetu,”amesema rais Cartes

Aidha, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameitaja hatua ya Paraguay kama siku nzuri kwa Israel na Paraguay kuendeleza urafiki wao

.Hata hivyo, Palestina inataka Jerusalem Mashariki iwe mji wake mkuu na eneo hilo ndilo kikwazo kikubwa katika kupatikana kwa amani kati ya Waisraeli na Wapalestina.

 

Bunge lamlima barua Mugabe
Machinga wapigwa marufuku barabara kuu

Comments

comments