Meneja wa klabu ya Crystal Palace, Alan Scot Pardew amekanusha taarifa za kuwasilisha ofa ya kutaka kumsajili beki na nahodha wa klabu ya Newcastle Utd, Fabricio Coloccini.

Pardew amesema kamwe hawezi kufanikisha usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 33, kutokana na kufahamu ugumu wa kumng’oa huko St James Park yalipo makao makuu ya klabu ya Newcastle Utd.

Hata hivyo, tayari meneja wa The Magpies Steve McClaren, ameshaweka wazi kupitia kituo cha radio cha shirika la utangazaji la Uingereza BBC, kuhusu mchezaji huyo raia wa nchini Argentina, ambapo alisema hana mpango wa kumuachia na kujiunga na klabu nyingine.

Balaa Gani Hili, Wilshere Nje Miezi Miwili
Kagame Cup 2015 Yaongeza Neema Azam FC